URAIA, DEMOKRASIA NA MAENDELEO
From KLAMediaWiki
URAIA KUHUISHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
MWANAHABARI: MBWANA RAJABU
WAKATI: 8.30 HADI 11.00 JIONI
ORGANIZER: SAHIBA SISTERS FOUNDATION-Tanzania WALIOHUDHURIA: 39 WANAUME 10 WANAWAKE 29
MNENAJI: SALMA MAULID
YALIYOTOKEA
Watanzania wengi nchini na Dunia kwa ujumla hawafahamu vema nini maana ya uraia kwa kuwa mipaka yake haieleweki vema. Hii hutoa fursa ya kitotambua haki zao za kimsingi, hasa akina mama kama uzawa, uongozi, na mahitaji mengine. Masuala ya uraia ni muhimu na yana sura mbalimbali, ambayo ni zaidi ya uchaguzi ambapo wengi huamini kuishia hapo.
Kwa mfano,katika Tanzania, endapo mwanamke wa kitanzania akiolewa na mgeni toka nje ya nchi, mume huyo hatambuliki kisheria kama mtanzania, ili-hali mwanamume wa Tanzania akioa nje ya nchi, basi mke huyo hutambulika kisheria kama mtanzania.
Je, haki na nafasi ya mwanamke iko wapi?
YALIOPENDEKEZWA
Kuna haja ya akina baba kujua haki za msingi za akina mama na watoto.
Pia kuna haja ya kuielimisha jamii kuhusu uraia.
Jamii pia ijishirikishe katika masuala mbalimbali yahusuyo uraia na mambo yafananayo.
Alamsik